\ talktz

Video mpya ya Jeniffer Lopez ni shiiiiida!!!!


Jlo ameachia video ya nyimbo yake mpya ya booty ambayo kamshirikisha mwanadada iggy azaela. Ebu icheki hapa uone mambo waliyofanya wawili hawa  yani ni sheeda…

(Video) Wafungwa miaka sita na bakora 91 kwa kucheza wimbo wa Pharrell


Iran: Wafungwa miaka sita na bakora 91 kwa kucheza wimbo wa Pharrell 'Happy'

Kundi la wasichana na wavulana sita wa Iran waliocheza wimbo wa Pharrell Williams ‘Happy’ na kisha video yao kusambaa kwenye mitandao mwezi May mwaka huu wamekamatwa tena rasmi na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela na bakora 91.

Hukumu hiyo inakuja ikiwa ni miezi kadhaa tangu walipokamatwa kwa kosa hilo na kuachiwa kwa muda baada ya watu mbalimbali duniani kukemea kwa nguvu kitendo hicho kwa kuwa waliamini vijana hao walikuwa wanajifurahisha tu.

Hata hivyo, kitendo hicho kilitafsiriwa kuwa kinyume na sheria za nchi hiyo hususani mavazi waliyokuwa wamevaa na aina ya michezo waliyoicheza.

Vijana hao walikiri kosa hilo na kueleza kuwa walirubuniwa na watu kuwa ilikuwa sehemu ya usaili wa kazi ya uigizaji jijini Tehran.

Muda mfupi baada ya hukumu hiyo kutajwa, mwanasheria wa aliyekuwa anawatetea vijana hao, Farshid Rofugaran ameeleza kuwa hukumu hiyo imesamehewa kwa mujibu wa sheria na kwamba itatekelezwa endapo vijana hao watarudia kosa kama hilo ndani ya kipindi cha miaka mitatu.

Picha: Mpiga picha anaeiwakilisha Tanzania katika Big Brother Africa 2014, Muigizaji huyu wa kike anaweza kutajwa pia

Waandaaji wa shindano la Big Brother Africa wameendelea kutangaza majina ya washiriki wa shindano hilo, na leo wametaja majina ya washiriki watatu akiwemo Idris kutoka Tanzania.

Kwa mujibu wa mtandao wa Big Brothe Africa, Idris Sultani ameeleza kuwa ana mikakati na anatumaini  washiriki wenzake watamgeukia yeye pale wanapotaka kuwa inspired au wanapokuwa katika wakati mgumu.

Hata hivyo, taarifa za awali ambazo hazijathibitishwa bado na waandaaji wa Big Brother zilimtaja Idris Sultani na muigizaji Irene Veda kuwa ndio watakaoiwakilisha Tanzania.

Baada ya Idris kutangazwa leo, taarifa hizo za awali zimepewa nafasi zaidi. huenda Irine akatangazwa hivi karibuni japo hakuna uhakika wa kutosha.

Washiriki wengine waliotajwa leo kuwa kati ya wanaowania ushindi katika shindano hilo lilopewa jina la ‘Hot Shots’ ni Goitse kutoka Uganda na Esther kutoka Uganda.

P Square kuachia albam ya 'Double Trouble' September 12

Kundi la mapacha wa Nigeria, P-Square limetoa kava ya albam yao ya sita ‘Double Trouble’ na wameweka wazi kuwa albam hiyo itatoka September 12.

Katika albam hiyo wasanii wengi wakubwa wameshirikishwa akiwemo Awilo Longomba, T.I, Jermaine Jackson, Don Jazzy na Dave Scott.Tayari wakali hao wameshatanguliza ngoma tatu kali kutoka kwenye albam hiyo ambazo ni pamoja Shekini, Ejeajo na Bring it On.

Diamond apiga mbili kwa mpigo, ashinda tuzo Australia na atajwa kuwania tuzo ya MTV Europe Music

Neema inazidi kumuangia Diamond Platinumz na leo amepata habari njema baada ya kutajwa kuwania tuzo ya MTV EMAs huku akipokea tuzo kutoka nchini Australia.

Diamond amewapa mashabiki wake habari njema za ushindi wa tuzo ya AAMA ya Australia kupitia tiketi ya collabo ya aliyopewa na Desert Eagle, wimbo unaoitwa ‘Everyday’.

“Ningependa niwajulishe kuwa kijana wenu nimepata tunzo nyingine toka Australia ya Collabo bora ya Mwaka toka kwenye tunzo za #AAMMA_Awards kupitia nyimbo niliyoshirikishwa na Desert Eagle iitwayo #EVERYDAY..... (jus wanted to inform you that, your favourite artist @Diamondplatnunz won another award from Australia on #AAMMA_Awards as best Collaboration song of the Year..).” Ameandika.Wakati huo huo, mtoto wa Tandale ametajwa kuwa moja kati ya wasanii wanaowania MTV Europe Music Awards mwaka huu huku akichuana na wakali wengine kutoka Afrika akiwemo Davido, Toofan (Togo) na Goldfish (Afrika Kusini).

Msanii mwingine wa tano akisubiria kutajwa baada ya mashabiki kumpekeza kutoka kwenye kundi la wasanii sita ambao ni Anselmo Ralph, Gangs of Ballet, Mafikizolo, Sarkodie, Sauti Sol na Tiwa Savage.

Aidha, majina yote ya wasanii wanaowania tuzo hizo yatatajwa September 16 ambapo upigaji kura utaanza rasmi.

Hongera Diamond Platinumz, Tanzania inazidi kutajwa kwenye majukwaa ya kimataifa.

NEW VIDEO:DULLY SYKES - TOGOLA

DULLY SYKES - TOGOLA

Dully Sykes a.k.a Mr. Misifa kaachia video mpya iitwayo 'Togola'.

Picha: Hulk Hogan 'Fake' aiteka Lagos, apata mapokezi na ulinzi wa kitemi


Vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti habari kuhusu uwepo wa mwanamieleka mkongwe, Hulk Hogan katika jiji la Lagos. Ingawa kwa muonekano anaonekana ndiye lakini inaelezwa kuwa mtu huyo sio Hulk Hogan halisi.

Mtu huyo ameonekana akizunguka mitaa akiwa juu ya gari huku umati wa mashabiki ukimfuata na amepewa ulinzi mkali wa polisi ambao ni vigumu kuamini kuwa ni kweli atakuwa fake.
Mitandao ya Nigeria imeeleza kuwa, Hulk Hogan halisi hajafika Nigeria na kwamba inawezekana kabisa kuna mtu amefanya mchongo huo ili kuwaibia watu.
 
Taarifa za Hulk Hogan Fake zimefananishwa na zile za PSY wa Gangnam Style aliyewahi kuingia nchini humo na kupewa mapokezi na matunzo ya daraja la kwanza kabla hajajulikana kuwa sio PSY halisi.
 
Kilichomuumbua PSY huyo ambaye ilikuwa vigumu kumtofautisha, ni pale PSY halisi alipoonekana akiga show Marekani siku hiyo hiyo.
Hapo hali ilibadilika Lagos kwa PSY aliyekuwepo na alikamatwa na vyombo vya usalama.
 
PSY halisi(kushoto), PSY fake (Kulia/mwenye koti jeusi)

SIMULIZI YA MAISHA ALIYOPITIA DIAMOND NA HISTORIA MBAYA NA BABAKE01. Diamond Platnumz aliachwa na baba yake
Diamond alizaliwa tarehe 2, October mwaka 1989 katika Hospitali ya Amana Dar es salaam. Akiwa na umri mdogo wazazi wake walitengana na baba yake kumuacha bila msaada wowote. Hapa chini huyo ndiyo baba yake diamond.

Diamond-Wema-Baba-yake


02. Chumba  kupangishwa ili kumsomesha
Baada ya wazazi wake kutengana, Diamond aliamia kwa bibi yake huko tandale na ilipofika muda wa yeye kwenda sekondari ilibidi bibi yake apangishe chumba kimoja ili Diamond aende shule na ikabidi alale chumba kimoja na bibi na mama yake.

Diamond-na-bibi-yake
03. Aliacha shule kwa kukosa Ada
Diamond alikua na akili darasani na alipomaliza elimu yake ya O’level ilikosekana pesa ya kumpeleka A’level na hapo ndio ilikua mwisho wa elimu yake.
diamond-utotoni-slider04. Diamond ameshafanya kazi viwandani, Kafanya kazi za kupigisha simu , kuuza mitumba na kuuza maji.
Kuna kipindi Diamond alikuwa akifanya kazi katika kiwanda cha mabegi kilichoko Mikocheni na kulipwa mashahara wa shilingi 2,000 kwa masaa 8.


Diamond-zamani
05. Mama yake alisaidia sana kutoka kwake
Mama yake alikuwa anampeleka kwenye talent show na kumsubiria hadi usiku mpaka aperform ndo wanarudi wote. Ndugu zake wengine waliona anamdekeza mwanae.

Profesa Jay aanzisha website yake, ataja siku ya kuzindua video za Kipi Sijasikia na Tatu Chafu

The heavy Weight MC, Profesa Jay ameanzisha website yake binafsi (official website) ambayo ina matukio mengi yanayohusu harakati ya muziki wake, nyimbo na video zote zinazomhusu.

Akiongea na Bongo Dot Home ya 100.5 Times Fm, Profesa Jay amesema kuwa ameamua kufanya hivyo baada ya kuona hitaji la kwenda na wakati na kwamba watu wengi hata walioko nje ya mipaka ya nchi wanataka kufahamu mwenendo wa muziki wake hivyo ameona ni vyema kuwapa sehemu ya kuvipata muda wowote.

“Nimeamua kuwa na website yangu kuzidi kujitengeneza, kujipackage na mtu aweze kukufikia kirahisi. Nimeona value yangu na nimeona wapi nilikosea, kwa muda mrefu watu wemekuwa wakiulizia website, kazi zangu watazipata wapi, wapi muziki wangu, wapi shows zangu…so kwenye website kutakuwa kuna kila kitu kitakachojiele. So kila kitu ntakachokuwa nafanya kitakuwa kinapatikana kwenye website yangu.” Amesema.

Katika hatua nyingine, profesa amesema kuwa atazindua video mbili za nyimbo zake ‘Kipi Sijasikia na Tatu Chafu’ pamoja na website yake Wikendi hii.

“Watu wakae tayari, kutakuwa na performance pale. Profesa Jay atakuwa anaperform, marafiki wangu ambao wananisapoti na tunasapotiana watakuwepo. Mastaa wengi pia watakuwepo kuona Profesa Jay amefanya nini. Kwa hiyo watu wakae tayari tutawapa information zaidi. Lakini by next week kama Ijumaa tutakuwa tunafanya uzinduzi.”

Kutembelea website ya Profesa Jay ingia www.profesajay.com

Picha: Diamond na Yemi Alade kurekodi wimbo pamoja

Diamond amekutana na mkali wa Johnny toka Nigeria, Yemi Alade wakati wa kureko msimu wa pili wa Coke Studio.

Wawili hao wanatarajia kurekodi kama pair ya muziki kwa ajili ya kipindi hicho ambacho huwakutanisha wasanii wengi wakubwa Afrika na kufanya muziki kwa pamoja huku wakiimba LIVE. Huenda kukawa na project kati yao siku za usoni.

#wonderment! With the infamous ubertalented six-abbs superstar Diamond @diamondplatnumz #iAmHumbled #thankYouCokeStudio, ForThe Opportunity God bless AFrica.. #cokeastudioafrica @cokestudioafrica @dresomes Nosa @chocolatecity Diamond has been singing your song all morning @audumaikori.” Ameandika Yemi kwenye Instagram na kupost picha akiwa na Diamond.Naye Diamond alipost picha kwenye instagram wakiwa wawili na kuandika, “Na dem ake Johny @yemialade , ushaelewa nini kinaendelea si eti????.. (jus me and Johny’s Girlfriend….You allready know what it is ryt???....Cc @yemialade.”

Wengine walitengeneza pair katika kipindi hicho ni Vannessa Mdee na Burna Boy (Nigeria), Joh Makini na Chidinma (Nigeria), na Shaa na Jacky Chandiru (Uganda).
 
Support : talktz | Shau Template | Mas
Copyright © 2011. talktz - All Rights Reserved
Template Modify by Shau
Proudly powered by Blogger